Azam FC na timu mpya kwenye ligi kuu ya Mwadui FC ya Shinyanga kesho usiku zitakwaana kwenye uwanja wa Azam Complex katika mechi ya kirafiki kujiandaa na ligi kuu.

Mashabiki wa soka nchini watapana nafasi kuiona mechi hii live kupitia moja ya chaneli za Azam TV.

Azam FC ambayo imepoteza wachezaji wake wengi walio na timu ya taifa itatumia mechi ya kesho kuwapa nafasi wachezaji ambao hawakupata nafasi kwenye mechi nyingi zilizopita huku kwa Mwadui FC timu iliyotoka sare ya 0-0 na Simba jana itatumia mechi hiyo kuendelea kuwaweka pamoja wachezaji wake ambao wengi ni wapya.

Wakati huo huo, wacheaji Ismail Adam Gambo na Omary Wyne wamesafiri kwenda Songea kujiunga na Majimaji ya huko kwa mkopo.

Hii ni nafasi muhimu kwa wachezaji hawa wenye vipaji toka Academy ya Azam FC kupata fursa ya kucheza ligi kuu na kupata changamoto mpya baada ya kutumia takribani miaka mitatu kwenye academy wakijifunza soka.

Wachezaji hawa pia ni wanandinga wa timu za taifa za vijana.

Picha: Lowassa Atembele Soko La Tandale Kwa Kushitukiza
Shelly-Ann Fraser-Pryce Kinara Wa Mita 100