Klabu ya Mwadui FC imekuwa ya kwanza kurejea Ligi Daraja la Kwanza baada ya kukubali kufungwa dhidi ya Maafande wa Jeshi la Magereza Tanzania Prisons, jana Jumanne (Mei 08).

Mwadui FC walikuwa nyumbani Mwadui Complex mkoani Shinyanga walikubali kupoteza mchezo huo kwa kufungwa bao moja kwa sifuri, ambalo liliizamisha rasmi timu hiyo, ambayo msimu ujao 2021/22 itashiriki ligi daraja la kwanza (FDL).

Baada ya mchezo huo nahodha wa Mwadui FC Joram Mgeveke alizungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa, licha ya kushuka ramsi na kutarajiwa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza, lakini michezo iliyosalia wataendelea kupambana ili wao kama wachezaji kujiuza sokoni.

“Inauma sana timu kushuka daraja, pamoja na hilo haitatuvunja moyo. Tutaendelea kupambana ili kujiweka sokoni dirisha la usajili litakapofunguliwa kwani tutaonyesha viwango bora.”

Mgeveke pia akafichua sababu ya timu hiyo kushuka daraja ni ilitokana na kikosi chao mwanzoni mwa msimu kukosa wachezaji wenye uzoefu na Ligi Kuu.

Mwadui FC inaburuza mkia wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa na alama 19, zilizotokana na michezo 30 waliocheza mpaka sasa.

Mukoko Tonombe kuikosa JKT Tanzania
Babu Tale: Wapuuzieni wanaosema naoa