Makamu mwenyekiti wa Young Africans Fredrick Mwakalebela amemjibu Mwenyejiti wa zamani wa Simba SC Ismail Aden Rage, kufuatia kauli yake aliyoitoa kuhusu sakata la kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison.
Mwakalebela amesema Rage hana nafasi kwenye sakata hili, na taarifa aliyoitoa kwa kuutaka uongozi wa Young Africans kuachana na kesi ya Morrison na kuendelea na mambo mengine haina mashiko.
Amesema mdau huyo ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa Chama cha soka nchini FAT kwa sasa Shirikisho la soka (TFF), ameshapitwa na wakati na endapo anataka kujua ukweli wa kesi ya mchezji huyo kama ipo CAS, amefute muhusika.
“Rage ameshapitwa na wakati na kama anataka kujua ukweli wa kesi yetu na Morrison huko CAS, basi amfuate Mchezaji wake Morrison atamuonyesha Document (Nyaraka) zote na kila kinachoendelea.” Amesema Mwakalebela.
Mwishoni mwa juma lililopita Mwakalebela alizungumza na waandishi wa habari akiwa jijini Mbeya na kueleza kuwa, uongozi wa Young Africans unaaamini kwamba haki yao ya mchezaji wao wa zamani Bernard Morrison itatendeka kwa kuwa kesi itasikilizwa baada ya FIFA kuwapa jaji atakayesikiliza kesi hiyo.
Morrison ambaye aliitumikia Young Africans kwa takribani miezi sita msimu uliopita, alijiunga na Simba SC msimu huu 2020/21 ambapo usajili wake ulileta mvutano mkubwa kiasi cha kufikishana TFF, na baadae alishinda kesi iliyothibitisha yupo huru kujiunga na timu yoyote baada ya kubaini mapungufu kwenye mkataba wake.