Bondia Hassan Mwakinyo ‘Champez’ ameeleza furaha yake na kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kulimaliza suala lake na kuondolewa adhabu ya kufungiwa kutoshiriki mchezo huo kwa mwaka mmoja na faini ya Shilingi milioni Moja.

Mwakinyo amezungumza hayo baada ya juzi Jumatatu (Novemba 27) Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) kumwondolea kifungo hicho walichomwadhibu Oktoba 10 baada ya kutopanda ulingoni kuzichapa na Julius Indongo wa Namíbia Septemba 29, mwaka huu akidai mapromota walikwenda kinyume na makubaliano yao.

“Kwanza namshukuru Mungu maana nilikuwa na imani ya kutokaa muda wote huo bila kupigana na mwisho amesikia ndoto yangu na pia BMT (Baraza la Michezo Tanzania) kupitia Wizara wamelisimamia hili na kulimaliza vizuri kwa faida ya michezo Tanzania.

“Nafikiri ilionekana haja ya kumaliza hili ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza michezo hapa nchini na nashukuru baada ya vikao vya maridhiano ya pande zote mbili, tumefanikiwa kulimaliza na sasa nipo huru,” amesema Mwakinyo.

Mifumo Utawala Bora wa Sheria iimarishwe - Wadau
Kevin de Bruyne kurudi Man City 2024