Kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa na mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia, @BoxRec leo Julai 26, 2021 imemtaja Bondia wa Tanzania, @HassanMwakinyo kuwa Bondia namba 1 barani Afrika na namba 37 duniani kati ya mabondia 2,050 wa uzani wa Super Welter.
Mwakinyo amefikia hatua hiyo kufuatia kufanya vizuri kwenye mapambano yake ya hivi karibuni.
