Bondia Hassan Mwakinyo amewataka mashabiki wake kukaa kwa kutulia kwani mambo mazuri zaidi yanakuja.

Mwakinyo Jumapili ya wiki iliyopita alimpiga bondia Kuvesa Katembo wa Afrika Kusini kwa pointi katika pambano lilofanyika Uwanja wa Jamhuri, jijini hapa.

Mwakinyo amesema anaendelea kujifua kuhakikisha anafanya vizuri katika mapambano yake yanayokuja ikiwemo lile la mwezi Juni mwaka huu.

“Najaribu kubadilisha kiwango changu kwa kushirikiana na makocha wangu, mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita tutaenda kuyarekebisha na niwaahidi mashabiki wangu mambo mazuri zaidi yanakuja, nategemea kupanda ulingoni mwezi wa sita,” amesema Mwakinyo.

Kuhusu mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani katika pambano la Jumapili, Mwakinyo alisema: รข coeBinafsi nimefurahi sana licha ya mvua lakini hawakutaka kuondoka nina deni hapa.”

Waziri wa Habari, Utamadini Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana alimpongeza Mwakinyo kwa kupata ushindi huo huku akidai serikali inajivunia kipaji chake.

Ziara ya kikazi: Rais Kagame kuwasili nchini Aprili 27
Young Africans yamsafisha Bernard Morrison