Bingwa wa mkanda wa WBC Africa uzito wa Super Welterweight Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo amefichua siri kwa kusema mpinzani wake kutoka nchini Angola Antonio Mayala, hakupasa kupigana naye.

Mwakinyo amefichua siri hiyo baada ya kumchakaza Mayala usiku wa kuamka jana Jumapili, jijini Dar es salaam, na kuendelea kuwafurahisha watanzania ambao siku zote wamekua wakimuamini.

Bondia huyo kutoka Tanga amesema Mayala hakustahili kucheza naye, lakini ilimlazimu, kufuatia mpinzani wake wa kwanza kuumia akiwa kwenye maandalizi.

“Hakustahili kucheza na mimi, nilipata alama 2 tu katika ranking za kidunia, kwa sababu nilikuwa nimemzidi katika ranking za boxing, nilipigana nae kwa sababu bondia wa kwanza aliumia. Ikabidi yule azibe nafasi.”

Hata hivyo Mwaknyo amesema hatua ya kubadilishiwa mpinzani dakika za mwisho ilimsumbua kimaandalizi, lakini alijiamini na kutambua umuhimu wa kwenda kushinda kwa ajili ya watanzania wote.

“Kubadilishiwa bondia dakika za mwisho, ilinisumbua lakini sikutaka kuiweka akilini kwa sababu ingenitoa mchezoni. Hasa ukizingatia wenzetu huwa wapo kwenye maandalizi muda wote, lakini ilibidi nishinde, hivyo nikapambana na kufanikiwa.”

“Boxing ni nzuri sana kwenda kupigana nje ya nchi kuliko ndani, kwasababu moja tu kwamba unaweza kupata bondia ambaye unalingana kwenye ranking, au aliyekuzidi ili ukimpiga upande zaidi na kujitengenezea nafasi ya kwenda kwenye level za kidunia.”

Familia China zaruhusiwa kuzaa watoto watatu
Rais Samia ampandisha cheo SACP Wambura, Aza Hilal atenguliwa