Kampeni ya Promosheni ya ngumi za kulipwa nchini, PAF Promotion Entertainment, imeweka wazi kuwa bondia Hassan Mwakinyo atapanda ulingoni dhidi ya Mkenya, Rayton Okwiri katika pambano la kuwania Mkanda wa Ubingwa wa IBA.

Pambano hilo linatarajia kupigwa Septemba 29, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar.

Promota wa pambano hilo, Alli Mndeme, amesema tayari wamekubaliana na IBA kwa Mwakinyo kuwania mkanda wa Ubingwa huo dhidi ya Rayton Okwiri kutoka Kenya.

Tupo hatua nzuri za maandalizi na tayari tumefikia makubaliano na Okwiri ambaye atacheza parnbano kuu dhidi ya Mwakinyo wakiwania mkanda wa ubingwa wa kimataifa wa IBA ambao makao makuu yake ni nchini Marekani.

“Kuhusu pambano litafanyika wapi, tumekubaliana kwamba safari hii moto utawaka katika Ukumbi wa Ubungo Plaza Septemba 29 huu, tuna mapambano mengine makubwa na yenye ushindani ambayo tutaweka wazi kadiri muda unavyokwenda.” amesema Mndeme

Pogba azusha kizungumkuti Juventus
Mbappe arudisha imani kwa mashabiki