Kampuni ya Promosheni ya Ngumi za Kulipwa, PAF Promotion imeweka bayana kuwa inapanga Jumatatu (Oktoba 09) kulipeleka mahakamani suala lao na Bondia namba saba kwa ubora nchini, Hassan Mwakinyo kwa lengo kujua watafidiwa vipi hasara ya Sh milioni 580 waliopata baada ya Mwakinyo kukacha pambano hilo.

Mwishoni mwa mwezi uliopita Mwakinyo alishindwa kupanda ulingoni katika pambano lililoandaliwa na kampuni hiyo, kufuatia madai aliyoyataja kwenye mitandao ya kijamii ya kukiukwa makubaliano yake na waandaaji wa pambano hilo ambalo alipaswa kupanda ulingoni dhidi ya Julius Indongo wa Namibia.

Promota wa pambano hilo, Karigo Godson Karigo amefichua kuwa wanakusudia keshokuwa Jumatatu kwenda mahakamani kwa ajili ya kufungua kesi ya madai ya fidia ya hasara waliopata baada ya Mwakinyo kugomea katika pambano lililopita kucheza tofauti na mkataba wake aliongia na kampuni hiyo.

“Sisi tunakusudia kwenda mahakamani siku ya Jumatatu kama kila kitu kitaenda sawa kwa sababu tumepata hasara ya shilingi milioni 580 ambazo hatujui tunafidiwa vipi kuzipata baada ya kugomea pambano kucheza.

Nalienda jana kuonana na mwanasheria na kuweza kujua pamoja kukamilisha taratibu kama tutaweza kuwahi kuweka sawa kila kitu basi Jumatatu (Oktoba 09), tutakuwa mahakamani ikiwa kinyume na hapo huenda ikawa Jumanne (Oktoba 10) maana lazima tukae na mwanasheria,” amesema Karigo

Vinicius Jr: Nilimshawishi Bellingham kuja hapa
Simba yafunguwa milango mdhamini tuzo za wachezaji