Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na michezo Dk. Harrison Mwakyembe ameagiza bondia Selemani Bangaiza afungiwe kushiriki mchezo huo mara baada ya kupigwa kwa Technical Knock Out (TKO) na bondia Andrew Moloney kutoka Australia jumamosi iliyopita.

Mwakyembe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache mara baada ya kutazama kipande cha video kilichomuonesha bondea huyo kunyosha mikono juu kusalimu amri ya pambano hilo bila kupigwa ngumi.

Mara tu pambano kuanza Mtanzania huyo alinyoosha mikono juu kuonesha kushindwa shindano hilo na kumfanya  mwamuzi alimalize pambano hilo.

Mwakyembe amesema mambo kama hayo yanarudisha nyuma michezo nchini Tanzania na kuamuru bondia huyo afungiwe ili iwe fundisho kwa wengine.

Hata hivyo kocha aliyeambana na bondia huyo, Anthony Rutha amesema bado hafahamu sababu ya Bangaiza kusalimu amri kwa sababu hakupigwa ngumi ambayo ilimchanganya na kumfanya ashindwe kuendelea na pamabano.

”Nimemuuliza sababu ya kuachia pamabano hanipi majibu ya kueleweka, Bangaiza ni kama amefanya ujanja maana ameacha pambano kiajabu ajabu” amesema kocha wake Rutha.

Aidha Bangaiza alipoulizwa alisema hajui kitu kilichotokea ila alikuwa anaona maluelue ndio sababu ya kuachia pambano hilo japo kuwa aliingia ulingoni kwa kengo la kuchukua ushindi.

 

 

Wananchi watakiwa kuunga mkono juhudi za Serikali.
TACIP yamkabidhi Pierre tiketi ya kwenda Misri Bungeni