Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge iliyoundwa kuchunguza sakata la Richmond, Harison Mwakyembe amesema kuwa ripoti iliyotolewa bungeni na kupelekea Edward Lowassa kujiuzulu uwaziri Mkuu ilikuwa ya kweli.

Mwakyembe aliyasema hayo jana Kyela, Mbeya wakati alipokuwa akiwahutumia wananchi katika mkutano wa kampeni ya kumnadi mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.

Alisema kuwa kamati yake ilibaini dhahiri bila kumsingizia Edward Lowassa ambaye hivi sasa ni mgombea urais wa tiketi ya Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, kuwa alishiriki katika ufisadi huo.

“Jamani naomba mniamini, tulichokisema kilikuwa sahihi. Na naomba Mwenyezi Mungu, kama tulisema uongo atupe adhabu leo,”alisema.

“Suala lililomtoa kwenye uwaziri Mkuu ni suala nililisimamia mimi. Jamani leo mimi nasema ukweli tulipitisha uamuzi wa kweli, baba tumekukuta kweli ukichomoa fedha ya wazee!” aliongeza.

Lowassa amekanusha kuhusika hata kidogo katika ufisadi wa Richmond akileza kuwa aliamua kujiudhuru kwa kuwajibika kama kiongozi wa serikali bungeni.

Wakati anajiunga na Chadema ambao awali walikuwa wakimtuhumu kuwa fisadi, Lowassa alieleza kuwa mkataba wa Richmond uliingiwa kwa shinikizo la viongozi wa ngazi za juu zaidi yake enzi hizo na kwamba yeye alitaka kuuvunja mkataba huo.

Lowassa: Yatakwisha Baada Ya Siku 60
Nay Wa Mitego, Roma Mkatoliki Kunogesha Kampeni Za Ukawa Jumamosi