Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Harisson Mwakyembe amesema Serikali haiwezi kuona Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinajiingiza katika siasa na kama TLS wanataka hivyo, basi Serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha Wanasheria.

Amesema kuwa kuwaingiza wanachama ambao wana nasaba za siasa au viongozi wa vyama vya siasa ndani ya TLS ni kuruhusu mgongano wa maslahi na yeye kama mwanasheria hawezi kulikubali jambo hilo.

Dkt Mwakyembe ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza na ugeni wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) uliomtembelea Ofisini kwake mjini Dodoma ukiongozwa na Rais wao, John Seka

“Kama Wizara hatujui mwelekeo wa TLS kwa sasa, hatuwezi kuiacha TLS ikijiingiza katika siasa halafu tukawaangalia tu. hatuna nia ya kuitawala TLS, ila tunawajibika kuwasimamia kwa kuwa Sheria yenu iko chini yetu, mkiharibu kwa lolote Wizara ndio yenye wajibu wa kuwatolea maelezo, katika hilo mnalotaka kulifanya sasa kuna mgongano wa maslahi, je nyinyi kama wanasheria hamkuliona au hamlioni?, amesema Mwakyembe.

Aidha, amesema kuwa Serikali haina shida na wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya siasa, ila ni lazima wafahamu kwamba viongozi wanaowachagua ambao ndio watakaobeba sura ya TLS na mwelekeo mzima wa chama, kama wanataaluma hawapaswi kuwa na nasaba za kisiasa ili kuepusha mgongano wa maslahi unapoweza kujitokeza

.Hata hivyo, amesema kuwa TLS sasa imekuwa haihitaji muangalizi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma nchi ilipopata uhuru, kwani ina wasomi wengi na vijana wengi wamekuwa wanachama pia na kwa hiyo ni bora kufanya mabadiliko ya sheria ili kuipa mamlaka TLS kujisajili kama NGO ambapo kiongozi yeyote wa chama cha siasa anaweza kuwa kiongozi wao.

 

Mauro Icardi: Nilikua Sahihi Kuihama FC Barcelona
Max Allegri Awageuzia Kibao Waandishi Wa Habari