Mwalimu wa shule ya Sekondari ya St. Magreth Wilayani Igunga Mkoani Tabora amekamatwa na boksi za pombe aina ya viroba 825 akiwa amevihifadhi katika duka lake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Selemani amemtaja mwalimu aliyekamatwa na maboksi hayo kuwa ni John Pastory (48).
Aidha, Kamanda Selemani amesema mwalimu huyo alikamatwa Machi 7, majira ya saa 5 asubuhi katika mtaa wa Mwayunge mjini Igunga.
Amesema kuwa baada ya jeshi la polisi kufanya upekuzi walifanikiwa kukamata vioroba hivyo vyenye thamani ya sh. milioni 77,136,000.
Vile vile, Kamanda Selemani amesema mwalimu huyo ndiye alikuwa msambazaji mkubwa wa pombe aina ya viroba wilaya ya Igunga.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mwayunge kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, Abel Shampinga amelipongeza Jeshi Polisi kwa kuwakamata wauzaji wa pombe za viroba na kuongeza kuwa yeye kama mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mwayunge hayuko tayari kuwatetea watu wanaovunja sheria za nchi

Askofu apongeza kuongezeka kwa sadaka kanisani
CCM kwa fukuta, wajumbe wawili wa Halmashauri kuu Taifa 'NEC' watiwa mbaroni