Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitarungu Wilayani  Serengeti, Thomas Marwa ametwangwa makonde na mwalimu mwenzake akiwa ofisini kwake.

Tukio hilo lilisababisha masomo na shughuli zingine kusimama shuleni hapo kwa muda ili kuweza kuupatia suluhu ugomvi huo.

Akizungumza kuhusu ugomvi huo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Thomas Marwa amesema kuwa, ameshambuliwa na mwalimu mwenzake Yaredi Amos kwa tuhuma kuwa anamfuatilia fuatilia kuhusu uwajibikaji wake katika majukumu yake.

“Nikiwa ofisini naendelea na majukumu yangu, ghafla mwalimu Amos aliingia Ofisini kwangu na kuanza kunishambulia kwa ngumi usoni, akihoji barua niliyomuandikia kuhusu uwajibikaji wake kazini,”amesema Marwa

Hata hivyo, kwa upande wake Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Serengeti, Juma Hamsini amesema kuwa amepokea taarifa tukio hilo na kuagiza hatua za kisheria na inizamu zichuliwe dhidi ya mwalimu huyo.

 

Maharamia kazi za filamu kufikishwa mahakamani
Wabunge Chadema wajiengua michuano ya mabunge EAC