Jana uongozi wa Dar24 Media chini ya kampuni yao mama ya DataVision International wamezindua kampeni  ya Tupo Pamoja Okoa Maisha ya Mariam iliyofanyika katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es salaam.

Kupitia kampeni hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mwalimu AJuwae ambaye ni mlezi wa shule anayosoma Mariam ya Kawe Ukwamani alipata nafasi ya kusimulia kisa na mikasa mbalimbali ambaye binti huyo ameipitia akiwa shuleni pamoja nakuelezea jitihada za kimasomo anazozifanya Mariam katika siku chache anazobahatika kuwa shuleni.

‘’Mariam ni mwanafunzi wa kipekee, pamoja nakusumbuliwa na matatizo hayo kwa miaka 9 hajawahi kuwa wa mwisho darasani’’ amesema Ajuwae.

Ameeleza kuwa  Mariam ni kati ya wanafunzi wanofanya vizuri darasani na hilo ni jambo ambalo linawashangaza hata walimu na wanafunzi wenzake kwani siku anazokosa shule ni nyingi kuliko siku anazohudhuria darasani.

‘’Akihudhuria hata siku 30,  usitegemee kuwa atafeli, atakuwa miongoni mwa waliofaulu” Amesema Mwalimu wa Mariam Ajuwae.

Aidha amewaomba wananchi na wadau kwa ujumla kuhamisika na kumchangia mtoto Mariam ili aweze kupata fedha za matibabu na kuelekea nchini India.

Kwani Mariam ana ndoto za kuwa daktari bingwa kitengo cha upasuaji ili kutimiza ndoto hiyo anahitaji msaada wa fedha za matibabu, kwani bila wadau na wananchi anaona ndoto zake zinafifia.

Ewe mtanzania mchangie Mariam kupitia Mlipa kwa Tigo Pesa, Mpesa au Airtell Money, aidha mchangie kupitia akaunti namba ya CRDB  0150021209500 jina la akaunti ni Data Vision International – Tuko Pamoja.

Askari mwingine wa JWTZ afariki dunia
Majaliwa awanusuru Viongozi 19 kutiwa mbaroni