Watu wanne, akiwemo mtoto mdogo, wametiwa mbaroni nchini Ufaransa, kufuatia kuuawa kwa kukatwa kichwa, mwalimu mmoja nje ya shule anayofundisha.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ameliita shambulio la kigaidi tukio hilo lililotokea katika kitongoji cha Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Paris.

Macron amesema muuaji, ambaye jina lake halijatajwa, alipigwa risasi na polisi, wakati wakijaribu kumkamata ambapo baadaye alikufa kutokana na majeraha.

Mwalimu huyo ambaye jina lake halikutajwa aliuawa kwa sababu alikuwa akifundisha uhuru wa kujieleza.

Ripoti zinaeleza kwamba, mwalimu huyo wa somo la historia, alikuwa amewaonesha wanafunzi wake picha, zenye katuni za Mtume Muhammad.

Mzazi mmoja ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, kabla ya kuonesha katuni hizo, mwalimu huyo alikuwa amewaomba wanafunzi wa Kiislamu watoke nje ya darasa, kwani hakutaka kuwaumiza hisia zao.

Tukio hilo lilitokea kwenye viunga vya mji mkuu, Paris, majira ya saa 11:00 jioni, karibu na shule anayofundisha mwalimu huyo.

Lissu amkumbuka Mzee Sitta
Bweni la shule ya Sekondari Uchira Islamic lateketea kwa moto