Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia mwalimu wa Shule ya Msingi Montfort, Eneza Andarson, 27, kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 10, kwa nyakati tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, SACP Wilbroad Mutafungwa, amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akifanya kitendo hicho cha unyanyasaji kwa mwanafunzi huyo mara kwa mara katika maeneo mbalimbali shuleni hapo, ikiwemo ofisini na hata kumfuata chooni.

“Mwanafunzi huyo ni mkazi wa Kihonda baada ya kumhoji alikubali kufanyiwa vitendo hivyo na mwalimu wake na aliweza kusimulia namna ambavyo alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo vya kikatili, wakati mwingine alikuwa anafanyiwa chooni na hata ofisini”, ameeleza Kamanda Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa, amewashauri wazazi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao , ikiwemo kuwakagua ili kujihakikisha kama hakuna vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa.

Lissu arejea Ubelgiji
Marekani: Mwanasheria Mkuu aunga mkono hoja ya Trump