Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara, linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Mkalapa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, kwa tuhuma za kumbaka binti (14), ambaye ni Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika shule anayofundisha.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nikodemus Katembo amesema tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2023 katika kijiji cha Mkalapa na mtuhumiwa huyo alikuwa ni Mwalimu wa kujitolea katika shule hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nikodemus Katembo.

Amesema, inasemekana Mwalimu huyo alimuita binti huyo nyumbani kwakwe na baada ya kuingia ndani alimkamata na kumziba mdomo ili asipige kelele, kisha kumfanyia kitendo hicho.

Kufuatia tukio hilo, Kamanda Katembo ametoa rai kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili kukomesha kabisa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Uamuzi wa Mahakama wasababisha raia kupigwa marufuku
Usihofie chochote zaidi ya makosa yako - Sheikh Kundecha