Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Migango iliyopo Wilayani Bukoba amemcharaza viboko mwalimu mwenzanzake mbele ya wanafunzi kwa tuhuma za wizi wa sahani tano pamoja na nusu kilo ya sukari iliyotolewa kwaajili ya mahafali ya wahitimu wa darasa la saba.

Katika Taarifa ya kulaani kitendo hicho, Kaimu Katibu wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Biharamulo, Joseph Lugumba amesema kuwa mwalimu mkuu, Mateso Musaku alimtandika viboko mwalimu wake, Hosea Masatu mbele ya wanafunzi tukio ambalo linalaaniwa na wazazi na uongozi wa CWT.

Amesema kuwa Mwalimu Masatu alidaiwa kuiba vitu hivyo siku moja baada ya kumalizika  kwa mahafali ya darasa la saba kwamba alipoulizwa alikiri kosa hilo, hivyo kupelekea adhabu ya viboko hivyo.

“Tunashauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kutumia mamlaka zilizomteua mwalimu mkuu huyo kuongoza shule hiyo amuwajibishe kwenye kwenye ngazi za kinizamu kwa maana amekiuka kanuni za uteuzi,”Lugunda

Hata hivyo, mwalimu Masaku alithibitisha kumchapa mwalimu mwenzake kwa madai kuwa alipata taarifa kwa mwalimu aliyetuhumiwa na hakutegemea kuwa tukio hilo lingeweza kuleta matokeo hasi katika jamii.

Video: Roberto aachia ngoma mpya akiwa na Vanessa Mdee
Beki wa zamani wa Stoke City afariki dunia