Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Dodoma imemfikisha Mahakama ya Wilaya ya Kongwa Mwalimu Mkuu wa Shule Msingi Karume kwa Tuhuma za kughushi vyeti vya Darasa la saba na kuviuza kwa shilingi 50,000.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo amesema kuwa lengo la Mwalimu huyo kughushi vyeti ni kuwauzia wanaojiunga na mafunzo ya kujitolea ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT.
Aidha Mwalimu huyo ameshaghushi vyeti kwa baadhi ya watu waliojukalikana kwa majina ya Mbaraka Juma na Elia Fred wote wakazi wa kata ya Kibaigwa Mkoani Dodoma.
Hata hivyo watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana baada ya kusomewa mashtaka yao na kusubiri kutajwa kwa kesi yao.
Sambamba na hayo yote Kibwengo ametoa rai kwa wananchi kuendelee kutoa ushirikiano na TAKKURU ili kutokomeza rushwa ambae ni adui wa haki.