Mgombe mwenza wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu amesema kuwa chama hicho kikiingia madarakani kitalipa fidia ya nyongeza ya mishara ya watumishi wa serikali ambao hawakupata kwa mujibu wa sheria.

Amesema hayo wakati akinadai sera za chama hicho katika mkoa wa Kilimanjaro ambapo pamoja na mambo mengine amejinadi kuwa atahakikisha kila mtanzania anapata bima ya afya kwa kuwa haki hiyo ni ya msingi na kwamba ili taifa liwe na maendeleo lazima watu wake wawe na afya njema.

“Watumishi wote walio chini ya Serikali tutakwenda kuwalipa ¬†fidia ya nyongeza ya mishahara yao ya miaka mitano waliostahili kwa mujibu wa sheria,” amesema Mwalimu.

“Tunakwenda kuhakikisha kila mtanzania anapata bima ya afya, ukijua kuwa wewe ni mtanzania lazima uwe na bima ya afya, bima ya afya ni haki ya msingi”, ameongeza Mwalimu.

Faida 10 za mafuta ya nazi zitakushangaza
Mwanamke aliyejikata mkono atupwa jela kwa utapeli