Mwalimu mmoja wa dini ya kiislamu nchini Indonesia, amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kuwabaka wanafunzi 13 wa kike kati ya mwaka 2016 na 2021.
Herry Wirawan, ambaye alikuwa mmiliki na mwalimu wa dini ya Kiislamu katika shule ya bweni, alikabidhiwa adhabu hiyo siku ya Jumanne, Februari 15, 2022.
Kulingana na ripoti ya polisi, wanane kati ya wanafunzi hao waliobakwa ni walio na umri wa kati ya miaka 12 hadi 16 na wote ni wajawazito huku akituhumiwa kuwanyanyasa kingono wanafunzi hao na kuwajeruhi vibaya baadhi yao.
Mienendo michafu ya Wirawan iligunduliwa Mei 2020, baada ya mzazi wa mmoja wa msichana walioathiriwa kugundua kwamba mwanawe ni mjamzito.
Serikali ya taifa hilo pia imeahidi kwamba itawalipa kila msichana aliyeathirika fidia ingawa viongozi wa mashtaka walimtaka mwalimu huyo kuhukumiwa kifo ama hata kuchinjwa kwa sababu ya madhara aliyowasababishia watoto hao.