Waziri  wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe, amewataka watendaji katika wizara hiyo kufanya kazi kwa weledi na ubunifu mkubwa, ili kuleta mageuzi katika wizara na kuongeza uwezo wa kuibua wawekezaji wapya wazawa nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wawizara hiyo, Waziri Mwambe amesema  kila mtendaji na wakuu wa idara katika wizara wanatakiwa kuhakikisha wanafanyakazi kwabidii na kuibua wawekezaji wapya.

“Kila mtumishi katika kitengo chake au idara afanyekazi kwa weledi mkubwa natamani mabadilikomakubwa na kwa muda mfupi kila mtendaji ujitambue na ujitafakari utalifanyia nini taifa lako,” amesema Mwambe.

amesema wizara ndiyo wahamasishaji na wawezeshaji wa shughuli za viwanda nchini,wanatakiwa kujitoa kwa nguvu zao zote na akili kuhakikisha sekta hiyo inakua na kuwanufaisha Watanzania.

Aidha amewataka watendaji na wasimamizi katika wizara kujenga utaratibu wa kuwapa motisha wafanyakaziwanaofanyakazi kwa uaminifu ili kuwaongezea motisha kwa kuwa jitihada hizo zitahamasisha utendajikazi katika wizara na kusimamia ushirikishwaji kwa watumishi wote katika majukumu.

“Katika hili hakikisheni ushirikishwaji kwa watumishi na kugawa majukumu sawa kwa watumishi wotena kutowabagua kitendo cha kuwabagua au kutoa majukumu kwa upendeleo itashusha morali kwawatumishi,” amesema.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Rikizi Shemdoe, amesema mkutano huo ni wa pili tangu kuzinduliwa kwa baraza hilo na utatumika kutathmini waliyokubaliana katika mkutano wakwanza na kuweka mikakati mipya ya kutekeleza kwa mwaka huu.

RC Kunenge kula sahani moja na wakandarasi Dar
Aron Kalambo: Mpigaji alikuwa fundi katika pigo lile