Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu saba akiwemo mchungaji wa kanisa la Calvary Assembies of God, Elia Mwambapa kwa ajili ya mahojiano kutokana na vifo vya watu 20 vilivyotokea jana usiku mkoani Kilimanjaro huku likimtaka Mtume Mwamposa ajisalimishe.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amethibitisha kushikiliwa kwa watu hao kutokana na tukio la vifo 20 vilivyo sababishwa na kukanyagana kwa watu wakiwa katika jitihada za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa lililofanyika uwanja wa Majengo.

Tukio hilo limetokea jana jioni, Jumamosi Februari 1, 2020, huku taarifa zaidi zikieleza kuwa zaidi ya watu 40 walikanyagana katika harakati hizo na kukimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

 

Magufuli atuma rambirambi vifo vya waumini 20 kwa mafuta ya Mwamposa
Video: Dude la Lugola kusomba vigogo, Marufuku ya Makonda Marekani, kuna siri hatujaambiwa