Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA kwa mara ya kwanza ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Amesema hayo katika kipindi cha XXL ya Clouds FM, alivyokuwa akifanyiwa mahojiano,Hata hivyo msanii huyo hakuweka wazi Chama chake cha Siasa na Jimbo ambalo atagombea.

“Kuhusu kugombea Ubunge mwaka huu 2020, Chama changu hakijaruhusu kuongea lakini ikifika muda nitasema, lakini nia ya kugombea Ubunge ninayo ila hata mambo ya kwamba Jimbo lipi nitagombea tusubiri”. amesema Mwana FA.

Hata hivyo ameweka wazi juu ya hali yake Kiafya mara baada ya Kukaa karantini kwa takribani siku 28 kutokana na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona ambapo amesema kuwa kwa sasa amepona.

Wakenya 18 wafia nje ya nchi kwa Corona

Visa vya Corona vyafika milioni 3 duniani

Namungo FC kumuongozea kandarasi Hitimana
Mkwasa awahimiza wachezaji Young Africans