Mwanamuzi  mkongwe wa bongo fleva Mwana FA amethibitisha kukutwa na ugonjwa wa Corona muda mchache baada ya meneja wa diamond Platnumz Sallam SK kuweka majibu yake hadharani kuwa yeye ameathirika na virusi hivyo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mwana FA amethibitisha hilo huku akiwapa moyo watanzania na kuwataka kuwa makini na ugonjwa huo

Amesema ugonjwa huo upo na unaweza kumpata  mtu yeyote hivyo watu wachukue tahadhari kulingana na maelezo yanayotolewa na wataalamu.

Amesema kuwa Ugonjwa huu sio wa kutisha sana na tumekuwa tunapata magonjwa mabishi zaidi ya haya na kama mwili wako uko vizuri ndani ya siku 7 hadi 10 virusi vinaisha kabisa

”Ndugu  Majibu ya vipimo vyangu vya Covid 19 yamerudi chanya. Inaudhi. Siumwi KABISA. Nipo sawa 100%. Na nimejitenga toka niliporudi ili kuepuka kuathiri wengine. Na kwa bahati hata watoto wangu sijakutana nao kabisa. Hawapo nyumbani.” Ameandika Mwana FA.

Mapema hii leo Meneja wa msanii mkubwa nchini Diamond Platnumz ambaye ni Sallam SK amekiri kukutwa na virusi vya corona na anaendelea kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

CORONA: Wageni kutoingia Bungeni Dodoma
Mkude kukutana na Ndayiragije, ampinga meneja wake

Comments

comments