Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Maasai Mara mwenye umri wa miaka 22 amefariki dunia baada ya jogoo wake kuwika kwa siku tatu mfululizo katika Kaunti ya Narok nchini Kenya.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, marehemu alifariki akiwa katika Hospitali ya Shepherd alikokuwa amelazwa akipoea matibabu baada ya kulalamikia maumivu kwenye eneo lililo chini ya tumbo lake na jogoo wake kuwika bila kukoma.
Jogoo huyo aliwika kutoka Jumamosi, Februari 19 hadi Jumatatu, Februari 21 na kuufanya usimamizi wa chuo hicho kumpeleka hospitalini.
Maafisa wa polisi walipata taarifa na kwenda hospitalini aliokuwa amelazwa na kumtambua mwananfunzi huyo alihudhuria sherehe na wenzake Februari 18, 2022 ambapo inadaiwa kuwa punde tu baada ya kupata mlo, mwananfunzi huyo alianza kulalamika kuhusu jogoo wake kuwika bila kuacha hali iliyomlazimu kutafuta matibabu.
Aidha Maafisa kutoka kwa Idara ya Upelelezo wa Jinai (DCI) tawi la Narok Kaskazini wanashughulikia suala hilo kwa lengo la kubaini mazingira na chanzo cha kifo hicho.