Mwanafunzi wa kidato ha tatu katika shule ya sekondari Kiagata, wilayani Butiama mkoa wa Mara Mwita Juma Machango, amemjeruhi kwa panga mkono wa kushoto mwalimu wake Majogoro John, baada ya kupewa adhabu kutokana na utoro.

Mwalimu huyo ameeleza kuwa awali alimwita mwanafunzi huyo ili ampatie barua ya kumuita mzazi wake kutokana na tabia yake ya utoro jambo ambalo mwanafunzi huyo alilikaidi.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Mara Joachim Eyembe, amethibitisha kumpokea mwalimu huyo ambaye amepelekwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Daniel Shillah, ambaye amethibitisha tukio hilo amesema jeshi la polisi linamshikilia mwanafunzi huyo kwa hatua za kisheria.

Lipumba aahidi kuigeuza Kyerwa kituo cha kimataifa cha biashara
Lori la mafuta lalipuka na kuua 23 katikati ya mji