Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia Said Shabani (39) kwa kosa la kumuua Naomi James (17), Mwananfunzi wa Shule ya Sekondari Kivukoni baada ya kumtuhumu kuiba kuni.

Akizungumza na Dar24Media Kamanda wa polisi mkoani humo, Henry Mwaibambe amesema kuwa tukio lilitokea katika msitu wa shamba la Miti, lililopo katika kata ya Nyankumbu, ambapo marehemu alikuwa na wenzake wawili wakitafuta kuni.

“Wakati wakiendelea kutafuta kuni kwenye shamba linalomilikiwa na Shabani ndipo mmiliki huyo alipoanza kuwakimbiza na marehemu alianguka na Shabani akamshambulia na kitu chenye ncha kali,” amesema Mwaibambe.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Geita.

Tanzania, Congo wapigwa marufuku kuingia Uingereza
Mcongo asajiliwa Simba SC