Jeshi la polisi katika Kaunti ya Migori nchini Kenya linamtafuta mtu mmoja kwa kosa la kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya Msingi Awendo.
Hatua hiyo imetokana na ripoti iliyowasilsishwa polisi kuwa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 13 ambaye ana tatizo la akili, alibainika kuwa ana ujauzito.
Mwanafunzi huyo alifikishwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo baada ya bibi yake kumtilia shaka, Jumatano wiki hii.
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi, ingawa msichana huyo ameeleza kuwa anaweza kumtambua mtesi wake, hakutoa maelezo ya kina kuhusu mambo yalivyokuwa kabla na baada ya kufanyiwa ubakaji.
Mkuu wa polisi wa Migori, Joseph Nthenge amesema kuwa wanaendelea na msako dhidi ya mtuhumiwa na wanaamini watafanikiwa kumpata.
Kiongozi Mkuu wa eneo hilo, Ezekiel Kokeyo, ameeleza kuwa ingawa madaktari hawakutaja tarehe kamili ya kutungwa kwa ujauzito huo, wameeleza kuwa unaweza kuwa na umri wa mwezi mmoja.
Chadema walia na mshahara wa Lissu
“Tumeanza msako kwa kushirikiana na jeshi la polisi na tutampa nafasi mwanafunzi huyo kuwatambua watuhumiwa ili waweze kufikishwa kwenye mikono ya sheria,” alisema Kokeyo.