Jopo la Mahakimu katika jimbo la Colorado nchini Marekani limesamehe kumhukumu kifo, James Holmes mwenye umri wa miaka 27 aliyeuwaua kwa risasi watu 12 waliokuwa wanaangalia Sinema ya Batman mwaka 2012.

Uamuzi huo umechukuliwa na jopo hilo la majaji 11 baada ya kubainika kuwa mtuhumiwa alikuwa na matatizo ya akili ya muda mrefu ingawa alikuwa anaendelea na masomo ya shahada ya uzamivu (PhD) katika mwaka aliofanya tukio hilo.

Hata hivyo, Jopo hilo lilioundwa na majaji lilikubaliana na waendesha mashtaka kuwa ingawa Holmes alikuwa na matatizo ya akili alitakiwa kuwajibika kwa vitendo vyake, hivyo wakamhukumu kifungo cha maisha jela bila kupata msamaha wowote hapo baadae.

James Holmes alikuwa akichukuliwa kama kijana mpole wakati anasoma shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu Cha Colorado ingawa alikuwa anakaribia kuondoka. Kwa mujibu wa ripoti ya FBI, Holmes hakuwa na rekodi ya makosa ya jina na hakuhusishwa na ugaidi.

Ilielezwa kuwa Holmes alikuwa amevaa ‘head phones’ na kuweka sauti kubwa ya muziki ili aisisikie sauti za vilio vya watu hao aliokuwa anawashambulia kwa risasi.

Benteke Atangaza Uadui Na Tim Sherwood
Ne-yo Kutua Kenya Kwenye Coke-Studio Mwaka Huu