Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Kitivo cha Afya, Azan Abubakary amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma akikabiliwa na mashtaka ya kufadhili ugaidi nchini.

Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mwajuma Lukindo, ilidaiwa kuwa mshtakiwa alituma kwa nyakati tofauti akiwa Dodoma ndani ya Mwezi Mei na Julai, jumla ya shilingi 413,000 kwa njia ya simu pesa kwenda kwa Mohamed Ibrahim kwa ajili ya kusaidia kutekeleza vitendo vya ugaidi.

Kutokana na vitendo hivyo, mshitakiwa amedaiwa kuvunja sheria chini ya kifungu cha 13 cha sheria ya kuzuia ugaidi namba 21 ya mwaka 2002.

Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwakuwa mahakama hiyo haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Awali, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mkoani Tabora baada ya mtandao wa kiintelijensia wa kupambana na ugaidi nchini kubaini kuwa anajihusisha na kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Afariki akiombewa kwa ‘nabii’ Arusha, akutwa hana nguo na nyusi
Arsene Wenger Amkataa Mathieu Debuchy