Mwanahabari maarufu wa Marekani, Grant Wahl (48), amefariki dunia wakati akiripoti michuano ya soka la Kombe la Dunia nchini Qatar kati ya Argentina na Uholanzi Desemba 9, 2022.

Wahl, alianguka ghafla wakati alipokuwa akitazama na akiwajibika katika mchezo huo wa Ijumaa usiku huku ripoti za awali zikionesha kuwa alipatwa na mshtuko wa moyo madai ambayo bado hayajathibitishwa.

Grant Wahl, katika picha yake iliyopigwa October 10, 2014. Picha ya Fred Kfoury III/Icon Sportswire/Corbis/Icon Sportswire/Getty Images.

Aidha, itakumbukwa kuwa Novemba, 2022 Wahl alizuiliwa kwa muda mfupi na mamlaka ya Qatar kwa kujaribu kuingia uwanjani akiwa amevalia shati la upinde wa mvua, kuunga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja LGBT.

Shirikisho la Soka la Marekani limesema limesikitswa na tukio la kifo cha Grant aliyekua akituma ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter kuhusu mechi ya Uholanzi na Argentina, kabla taarifa ya kifo chake kutangazwa.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 11, 2022
Wavamia Mochwari, waiba mwili wa marehemu