Mwanahabari wa Uholanzi amehudhuria mkutano wa siri wa Baraza la Mawaziri wa Ulinzi Mataifa ya Jumuiya ya Ulaya (EU) kupitia mtandaoni bila idhini.

Kwa mujibu taarifa za shirika la RTL Nieuws, mwanahabari Daniel Verlaan alitumia nywila ya tarakimu 6 ambapo aligundua tarakimu 5 za mwanzo kupitia picha iliyochapishwa mtandaoni na Waziri wa Ulinzi wa Uholanzi Ank Bijleveld.

Baada ya majaribio ya mara kadhaa na kufanikiwa kujiunga na mkutano huo, Verlaan, aliwapungia mkono kwa kuwacheka Mawaziri.

Mwakilishi wa EU wa masuala ya nje na sera za kiusalama Josep Borrell ambaye alikuwa akiongoza mkutano huo alimuuliza, “Unajuwa kuwa umeingia mkutano wa siri bila idhini?”

“Ndio, naomba samahani. Mimi mwanahabari wa Uholanzi. Mniwie radhi kwa kuingilia mkutano wenu. Naondoka sasa.”amesema Verlaan

“Unafahamu kuwa hili ni kosa ama sivyo? Itakuwa vyema kujiondoa kabla polisi hawajafika.”Borrell alimwambia mwanahabari huyo

Afisa mmoja wa EU aliarifu kuwa mkutano ulimalizika. Pia aliongezea kusema kuwa kitendo cha kuingilia mkutano bila idhini ni kinyume cha sheria na ataripoti kwa mamlaka husika.

Namungo FC wamkuna kocha Morocco
Mkwasa akataa ubingwa VPL

Comments

comments