Mwanaharakati maarufu nchini Kenya, Caroline Mwatha amefariki dunia mara baada ya kutoa ujauzito wa miezi mitano.
Taarifa ya Uchunguzi iliyotolewa na jeshi la Polisi nchini humo imesema kuwa kifo cha mwaharakati huyo maaarufu kilisababishwa na kitendo cha utoaji wa ujauzito wa miezi mitano.
Mara ya mwisho kwa mawanaharakati huyo kuonekana hai ilikuwa Jumatano ya wiki iliyopita kabla ya mwili wake kugunduliwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha City Mortuary jijini Nairobi.
Caroline Mwatha ni mwanaharakati aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la haki la kijamii katika kitongoji cha Dandora jijini Nairobi, shirika linaloshughulikia matukio ya mauaji ya kiholela yaliotekelezwa na maafisa wa polisi hususani katika vitongoji vinavyoshuhudia uhalifu mkubwa jijini Nairobi.
Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, George Kinoti imesema kuwa makachero wanaamini mwanaharakati huyo alifariki wakati alipokuwa akitoa ujauzito Jumatano ya wiki iliyopita, (Februari, 6), siku ambayo alionekana kwa mara ya mwisho akiwa hai.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya wapelelezi, imeongeza kuwa marehemu alikuwa kwenye mazungumzo ya simu ya mara kwa mara na mwanaume mwingine ambaye si mumewe kuhusu ujauzito huo.
-
Bilionea wa dawa za kulevya ‘El Chapo’ akutwa na hatia
-
Ughaibuni: Mtanzania akamatwa na dawa za kulevya tumboni
-
Mpinzani DRC aandika barua nzito kutaka uchaguzi urudiwe
Watu sita, wanashikiliwa na jeshi la polisi akiwemo mtu huyo aliyekuwa akiwasiliana na marehemu, mmiliki wa kituo cha afya kinachodaiwa alifariki ndani yake na dereva wa gari ya kukodi (Uber) ambapo mpaka sasa uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea.