Mwanaharakati wa mazingira, Gerald Bugurube kutoka Tanzania na Clovis Razafimalala wanatarajia kukabidhiwa tuzo ya Ujerumani kwa Afrika kutokana na juhudi zao za kutunza maliasili za nchi zao.
Tuzo ya Ujerumani kwa Afrika (German Africa Award) inayotolewa kila mwaka kwa watu walioonyesha mfano katika sekta ya kutunza mazingira, mwaka huu imewaendea Gerald Bigurube kutoka Tanzania na Clovis Razafimalala wa Madagascar.
Aidha, watu hao wawili wamesifiwa kwa kujitolea kunusuru maliasili katika nchi zao. wanaharakati hao wa mazingira wanakabidhiwa tuzo hiyo Ujerumani.
Kwa miaka 44, Gerald Bigurube, Mtanzania mwenye umri wa miaka 66 amejitolea maisha yake kuwaokoa wanyama wa porini pamoja na mazingira asilia nchini mwake.
Hata hivyo, kwa muda mrefu amekuwa mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa za Wanyama Pori Tanzania, TANAPA aliongoza mapambano dhidi ya majangili, na alianzisha juhudi za ujirani mwema baina ya mamlaka za kuhifadhi wanyamapori na jamii zinazoishi karibu na mbuga, pamoja na utalii ambao ni mojawapo ya nguzo muhimu za uchumi wa Tanzania.
-
Urusi yateka meli za Ukraine, yaziba njia ya bahari
-
Ziwa Victoria lazidi kuwa hatari, wengine 14 wafa maji
-
Watunisia kuandamana kupinga ugeni wa Mwana wa mfalme wa Saudi