Mahakama nchini Saudi Arabia imemhukumu mwanamke mwanaharakati wa haki za binadamu, Loujain al-Hathloul kutumikia kifungo cha miaka sita.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mahakama ya kupambana na ugaidi ya Saudi Arabia imemkuta al-Hathloul na hatia ya uchochezi wa kuleta mabadiliko, akifuata ajenda ya kigeni na kutumia mtandao wa intaneti kuharibu utulivu wa umma.
Al-Hathloul amekuwa jela tangu mwaka 2018 baada ya kukamatwa pamoja na wanawake wengine zaidi ya 12, raia wa Saudi Arabia ambao ni wanaharakati wa haki za binadamu.
Alikuwa akishinikiza kuwepo mageuzi kama vile sheria ya mwanaume kumsimamia mwanamke na kuwaruhusu wanawake haki yao ya kuendesha magari.
Kesi ya mwanamke huyu imekosolewa na wataalam wa haki za binadamu wa UN, makundi ya haki za binadamu na wabunge wa Marekani na Umoja wa Ulaya.