Mwanajeshi wa Uganda aliyempiga risasi na kumuua Waziri wa Leba, Ajira na Mahusiano ya Viwanda nchini Uganda, Kanali mstaafu Charles Okello Engola ametambuliwa kwa jina la Private Wilson Sabiiti.

Taarifa kutoka nchini Uganda zinasema Mwanajeshi huyo, alikuwa ameagizwa na kikosi kazi cha ofisini kwake kutoa ulinzi kwa Waziri huyo mwezi mmoja uliopita (Aprili, 2023).

Private Wilson Sabiiti, aliyetekeleza mauaji ya Waziri na kisha kujiuwa.

Katika tukio hilo, lililotokea nyumbani kwa Kanali Engola siku ya Jumanne asubuhi (Mei 2), Private Sabiiti pia alimjeruhi msaidizi wa Waziri Mkuu, Luten Ronald Otim ambaye kwa sasa anapokea matibabu katika Hospitali ya Mulago iliyopo jijini Kampala.

Mwanajeshi huyo anaripotiwa kufyatua risasi hewani huku akizunguka katika eneo la mtaa Kyanja jijini Kampala kabla ya kujiua hapo baadaye.

Mtibwa Sugar hali si shwari
Jose Mourinho akataa kazi jijini London