Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ametaja baraza lake la mawaziri huku akimteua Afisa wa jeshi kushika nafasi nyeti katika serikali yake.

Waziri mpya wa fedha ni Sibusiso Moyo, jenerali aliyetangaza katika televisheni ya taifa hilo wiki mbili zilizopita kwamba jeshi limechukua udhibiti.

Aidha, mwingine aliyeteuliwa katika nafasi ya uwaziri ni pamoja na Mkuu wa jeshi la anga, Perence Shiri ambaye ataongoza wizara ya kilimo.

Hata hivyo, Mnangagwa aliapishwa wiki moja iliyopita kufuatia kujiuzulu kwa alikuwa Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe.

Wabunge Chadema wazidi kusota rumande
Video: Walisubiri mpaka nife ndio waje kuniona?- Lissu