Wakati joto la uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likizidi kupanda, Hawa Mniga amekuwa mwanamke wa kwanza kuchukua fomu ya kuwania urais wa shirikisho hilo.

Hawa amechukua fomu hiyo ili kupambana rais wa TFF anayemaliza muda wake, Wallace Karia ambaye alichukua fomu ya kuwania tena nafasi hiyo Juni 8.

Mwanamke huyo ambaye ni mtumishi wa umma, alifika ofisi za  TFF  leo Ijumaa saa 5:00 asubuhi kisha kuingia moja kwa moja ndani kuchukua fomu.

Hadi sasa idadi ya waliochukua fomu ya urais imefika nane huku wengine wakiwa ni Karia, Deogratius Mutungi, Ally Mayay, Evans Mgeusa, Oscar Oscar, Tarimba Abbas na Zahir Mohammed Haji.

Kesho Jumamosi (Juni 12) ndio mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu.

Zahera: Nipo tayari kuisaidia Young Africans
Azam FC: Tunamaliza kimya kimya