Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa Wagonjwa wanne walidungwa sindano ya virusi katika kituo cha utafiti Kaiser Permanente mjini Seattle, Washington.
Chanjo hiyo haiwezi kusababisha Covid-19 lakini ina jeni la virusi ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa.
Wataalamu wanasema itachukua miezi mingi kujua ikiwa chanjo hii, au utafiti mwingine, utafanikiwa.
Mtu wa kwanza kujitolea kupata dozi ya kwanza ya utafiti huo siku ya Jumatatu ni mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa Seattle Washington.
“Hii ni fursa ya kufurahisha kwangu mimi kuweza kufanya kitu fulani,”alisema mama huyo aliyetambuliwa kama Jennifer Haller katika mazungumzo na shirika la habari la AP.
Chanjo hii huenda ikasaidia mwili kujitengenezea mfumo wake wa kinga wa kupigana na ugonjwa halisi.
Waliojitolea Kila mmoja atadungwa sindano mbili za virusi kwa ujumla, baada ya siku 28, kwenye mshipa wa sehemu ya juu ya mkono.
Aidha imeelezwa kuwa hata kama vipimo vya awali salama vimefanikiwa, bado inaweza kuchukua hadi miezi 18 kuweza kuwa na uwezekano wowote wa chanjo kuweza kupatikana kwa umma.