Mwariadha wa kike maarufu wa Afrika Kusini, Caster Semenya ameripotiwa kufunga ndoa ya kimila na na mwamamke mwenzake wikendi iliyopita.

Kwa mujibu wa Sport24, Semenya na mpenzi wake wa muda mrefu akliyetajwa kwa jina la Violet Raseboya walifanya ndoa ya kimila ktika eneo la Dikgale, Limpopo.

Semenya

78

Ingawa mwanariadha huyo alijitokeza na kukanusha taarifa hizo, gazeti la The Daily Sun lilienda mbali na kueleza kuwa mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 24 aliwatuma wazazi wake kujadili kuhusu mahari. Mwisho wazazi wake wanadaiwa kulipa kiasi cha R25000 za Afrika Kusini.

Semenya aliwahi kushinda medali ya fedha kwa mbio za mita 800 mwaka 2012 katika mashindano ya Olympics yaliyofanyika jijini London Uingereza.

Ray C: Nimefilisika, Nimekimbiwa
Home Shoppinga Center Yajitokeza Kujibu Tuhuma Za Kukwepa Kodi, wizi