Mahakama ya Afrika Kusini imemuongezea hukumu ya miaka 13 na miezi 6 jela mwanariadha mlemavu wa Afriika Kusini, Oscar Pistorius kwa kumuua mpenziwe, Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao 2013, baada ya kudhani kuwa alikuwa mwizi.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa kifungo cha miaka sita alichopewa mwanariadha huyo kwa kumuua Reeva Steenkamp kilikuwa hafifu mno.

”Wazazi wa Bi Steenkamp walijawa na hisia wakitazama hukumu hiyo wakati ikitolewa”, na kusema kuwa sasa wanahisi haki ya mwanao imefanyika, msemaji wao.

”Sasa anaweza kulala mahali pema peponi”, amesema Tania Koen

”Lakini wakati huohuo , watu wanahisi kwamba wamefika mwisho , ukweli ni kwamba wataishi na majonzi ya kumpoteza Reeva kila siku”, alisema bi Koen.

Rufaa ya mahakama ya juu mjini Bloemfontein imempatia Pistorius kifungo kisichopungia miaka 15 kwa mtu ambaye ameua nchini Afrika Kusini huku akiwa amehudumia miaka michache tayari.

Tshabalala atamani kutimkia Kenya
Robson de Souza atupwa jela miaka tisa