Mwanasayansi raia wa Uingereza maarufu duniani, Prof Stephen Hawking amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76 familia yake imetangaza.
Mwanasayansi huyo alikuwa mwandishi mzuri wa vitabu kadhaa maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).
Aidha, Watoto wake, Lucy, Robert na Tim, wamesema kuwa walikuwa wanampenda sana baba yao, lakini hawana namna.
“Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi.”wamesema watoto hao
Stephen Hawking alipokuwa na miaka 22 pekee aliambiwa na madaktari angeishi miaka mingine miwili pekee baada ya kugundulika anaugonjwa wa mfumo wa NEVA ambao ni nadra sana kutibika.
Hata hivyo, dakika za mwisho Ugonjwa huo ulimfanya kulemaa na kulazimika kutumia kiti cha magurudumu
-
Uingereza yainyooshea kidole Urusi
-
Trump amfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Nje
-
Uchaguzi wa rais kurudiwa Siera Leone