Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi amewaonya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutowabugudhi wabunge wa viti maalum kutoka chama hicho.

Profesa Kilangi amesema, mchakato wa wabunge wa viti maalum kutoka CHADEMA umefuata Sheria na Katiba, hivyo hawapaswi kubugudhiwa.

Awali, Spika wa Bunge Job Ndugai alisema, kanuni za Bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao na kuahidi kufanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Kuhusu wabunge 19 wa viti maalum kutoka CHADEMA, Ndugai amesema wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao, walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu.

Aidha, Spika Ndugai amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo iliyompa majina ya wabunge wa viti maalum na kazi yake ni kuwaapisha wabunge hao na tayari ameshafanya hivyo Novemba 24, mwaka huu jijini Dodoma.

Leo Novemba 27, Kamati kuu ya CHADEMA taifa inatarajiwa kutoa maamuzi ya pamoja juu ya wabunge wa chama hicho wanaodaiwa ‘kusaliti msimamo wa chama’.

Spika Ndugai mgeni rasmi maadhimisho ya walemamvu
Simba SC kutinga Jos, balozi Bana aipa baraka