Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Zanzibar, Othman Masoud  ameshauri Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kujiuzulu kwa sasa na kumuachia Jaji Mkuu kuunda Kamati Maalum.

Akiongea katika kongamano la wazi juu ya changamoto zilizojitokeza baada ya kufutwa kwa uchaguzi Mkuu Zanzibar lililoandaliwa na Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Othman alieleza kuwa baada ya Dk. Shein kujiuzulu, Jaji Mkuu anapaswa kuunda Kamati itakayofanya uchunguzi kuhusu uhalali wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.

Alishauri kuwa endapo kamati hiyo itakayoundwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu itabaini kuwa hakukuwa na uhalali wa kufutwa kwa matokeo hayo ya uchaguzi, itabidi wawajibishwe kisheria.

Kwa upande wake wakili wa kujitegemea, Fatma Karume alishauri kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi ili kuepuka migogoro katika chaguzi nchini.

Chanzo: Nipashe

Magufuli akiahidi anatekeleza; Ujenzi wa Flyovers waanza kwa vitendo
Walichozungumza Lowassa na Maalim Seif walipojifungia Dodoma