Mwanasheria wa zamani wa Raisi wa Marekani, Donald Trump amefikishwa mahakamani na kukiri hatia ya matumizi mabaya ya fedha za umma na uvunjifu wa sheria za uchaguzi katika mahakama ya New York.

Michael Cohen amekiri kuhusika na miamala ya fedha kwa mcheza filamu za ngono aliyekuwa na uhusiano na raisi Trump ili kumziba mdomo.

Katika kipindi cha utumishi wake kama mwanasheia wa raisi, Cohen anatuhumiwa kuandaa malipo kwa mwigizaji wa sinema za ngono, Stormy Daniels, mnamo mwaka 2016.

Aidha, mwanasheria huyo alikuwa chini ya uchunguzi maalum kutokana na tuhumza zilizokuwa zikimkabili za kuwepo uwezekano wa udanganyifu dhidi yake juu ya masuala ya benki na ushuru.

Hata hivyo, mwanasheria huyo amekata rufaa katika mahakama ya Manhattan dhid ya tuhuma zinazomkabili kuwa alikiuka sheria za uchaguzi, na kudai kuwa alifanya hivyo kwaajili ya maslahi ya mgombea.

 

Video: Nani anasema ukweli kati ya NEC na Chadema, DC matatani
Jeshi la Polisi laomba msamaha