Katika hali isiyotegemewa, mwanasiasa mmoja mkubwa nchini Ujerumani amependekeza kuwa askari wa nchi hiyo waruhusiwe kuwapiga risasi wakimbizi wanaoingia nchini humo bila vibali.

Frauke Petry ambaye ni Kiongozi Mkuu wa chama cha mlengo wa kulia cha Alternative for Germany aliliambia gazeti la Mannheimer Morgen kuwa anapendekeza askari kuchukua hatua hiyo ikiwa kama njia ya mwisho ya kutatua tatizo la kukomesha wakimbizi kuingia nchini humo bila kibali.

Frauke Petry, kiongozi Mkuu wa chama cha Alternative for Germany

Frauke Petry, Kiongozi Mkuu wa chama cha Alternative for Germany

Pendekezo hilo la mwanasiasa huyo mbishi linakinzana na sheria ya Ujerumani ambayo hairuhusu wakimbizi kushambuliwa na askari.

Kauli ya mwanasiasa huyo imepingwa vikali na wanasiasa wenzake pamoja na makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu.

 

Rais Magufuli akosolewa kwa kutohudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika, Ikulu yajibu
My Story: Nilivyojikuta Naupenda ukimwi alioupata mpenzi wangu na kilio chake