Kupitia andiko lake katika mtandao wa kijamii, mfungwa wa kisiasa, Viktor Babariko amesema Mwanasiasa mwenzake wa upinzani alieko gerezani nchini Belarus, Maria Kolesnikova amelazwa katika kitengo cha Wagonjwa mahututi.
Mwanasiasa huyo, Kolesnikova (40), alifanyiwa upasuaji ambapo andiko la Babariko kwenye ukurasa wake huo wa mtandao wa Twitter, limeelezea hali hiyo bila kutoa ufafanuzi na bado hakuna maelezo rasmi juu ya kulazwa kwake.
Kuwekwa kwake gerezani kunafuatia kutofautiana na mtawala wa muda mrefu wa Belarus, Alexander Lukashenko Pamoja na Sventlana Tikhanovskaya, Kolesnikova anachukuliwa kiongozi wa upinzani wa Belarus dhidi ya .
Wanawake hao wawili waliongoza maandamano ya nchi nzima mwaka 2020, kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka huo, ambamo Lukashenko alijitangaza mshindi.