Mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Afrika kusini, Shiraaz Mohamed aliyekuwa ametekwa nyara nchini Syria kwa zaidi ya miaka mitatu amerejea nyumbani jana baada ya kuachiwa huru.

Mohamed ambaye ni mpigapicha wa kujitegemea alitekwa nyara Januari 10, 2017, wakatati akiondoka katika nchi hiyo iliyoharibiwa kwa vita kuingia nchi jirani ya Uturuki.

Alikamatwa katika hospitali moja inayosimamiwa na shirika moja la hisani lenye makao yake nchini Afrika kusini ‘Gift of the Givers’ katika mji wa Darkouch, kilomita 60 kutoka Aleppo, mji mkuu wa pili nchini Syria.

Familia ya mpigapicha huyo imethibitisha kurejea kwake japo mazingira ya kurejea huko bado hayajawekwa wazi huku wizara ya mambo ya kigeni ya Afrika kusini ikisema ilikuwa ikishughulikia mazungumzo ya kuachiwa kwake tangu siku ya kwanza.

Na msemaji wa wizara hiyo ametoa taarifa kuwa, ni furaha kubwa kwakuwa Mohamed amerejea nyumbani akiwa salama.

DC Same atangaza kiama Polisi wenye urafiki na wahalifu, atoa siku 30 kusalimisha silaha
RC Mwanri awakabidhi watoto waliopotea kwa wazazi wao